Dodoma FM

Sekta ya madini ni kiungo muhimu katika ukusanyaji mapato.

1 March 2022, 3:34 pm

Na; Victor Chigwada.

Sekta ya madini Jijini Dodoma imekuwa kiungo muhimu katika nyanja ya ukusanyaji mapato licha ya baadhi ya migodi pamoja na jamii ya maeneo husika kutokunufaika kwa kiasi kikubwa.

Wananchi wa kijiji cha Nholi Kata ya Mpalanga wamesema kuwa mgodi wa Dhahabu uliopo kijijini hapo umekuwa chanzo kikuu cha Mapato kwa Wilaya ya Bahi na mkoa lakini bado wameshindwa kunufaika kikamilifu na mapato hayo.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Baraka Ndahani ameeleza kuwa licha ya mapato makubwa yanayo kusanywa lakini hakuna uwiano wa maendeleo ya wananchi na mapato hayo

Pamoja na ukusanywaji wa mapato ya kutosha katika mgodi wa Nholi bado kumekuwa na changamoto zinazo ukabili mgodi huo

Bw.Renatusi Lukumila ni mtendaji na mkemia mkuu katika mgodi huo amesema kuwa kukosekana kwa vifaa na wataalamu wa kuwasaidia kufanya utafiti wa miamba ni moja ya changamoto inayowakabili

Bw.Lukumila ameongeza kuwa mgodi wa Nholi umekuwa na mchango mubwa katika Wilaya ya Bahi na Jiji kwa ujumla hali iliyopelekea Serikali kuupongeza kwa hatua kubwa ya uzalishaji mapato

Taswira ya habari imezungumza na Afisa madini mkoa wa Dodoma Bw.Mchagwa Malwa ambaye mekiri pamoja na uwepo wa migodi kadhaa jijini hapa lakini mgodi wa Nholi ndiyo unaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu na mapato

Aidha Bw. Malwa ameongeza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutoa elimu kwa wachimbaji na kuwaomba waendelee kuwatumia wataalamu wa JIOLOJIA (GST) ili kuwapatia taarifa za awali juu ya uelekeo wa miamba ya madini

Inakadiliwa kwa asilimia 85 hadi 90 dhahabu inayozalishwa Jijini Dodoma inatokana na mgodi wa Nholi ambao kwa mwaka jana unakadiliwa kutoa makusanyo ya fedha takribani Bilioni ishirini