Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuwapa ushirikiano watu wenye ulemavu

16 February 2022, 3:55 pm

Na; Thadei Tesha.

Jamii imetakiwa  kuelewa kuwa wapo baadhi ya watu wenye ulemavu ambao wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jamii kutokana na kupewa ushirikiano kutoka katika jamii.

Akizungumza na taswira ya habari katibu mkuu wa shirikisho la watu wenye ulemavu mkoa wa dodoma mchungaji Kenneth Mlawi ameitaka jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa watu wenye ulemavu ambao kwa namna moja ama nyingine wameweza kuanzisha fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi.

Aidha ameongeza kuwa taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi wanaweza kuanzisha vituo kwa ajili ya kutoa fursa mbalimbali ikiwemo elimu mafunzo maalum kwa ajili ya kundi hilo ili watu wenye ulemavu nao wawe sehemu ya jamii inayopata fursa kama ilivuyo kwa makundi mengine.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kundi la watu wenye ulemavu limekuwa likikabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo ipo haja kwa taasisi mbalimbali pamoja na watu wanaojiweza kiuchumi kusaidia kutoa fursa kwa ajili ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Insert3…………………wananchi

Watu wenye ulemavu wamekuwa wakiijingiza katika fursa mbalimbali za kujikwamua kiuchumi ambapo wamekuwa wakijipatia kipatio chao cha kila siku hivyo ipo haja kwa jamii kuendelea kutoa mchango kwa kundi hilo kama viongozi mbalimbali wanavyosisitiza.