Dodoma FM

Jamii yatakiwa kujenga vyoo bora ili kuepuka matatizo ya kiafya

3 December 2021, 10:20 am

Na; Benard Filbert.

Wito umetolewa kwa jamii kujenga vyoo bora ili kuepuka adha ya kiafya ambayo inaweza kujitokeza.

Wito huo umetolewa na afisa afya wa Jiji la Dodoma Abdallah Mahiya wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utekelezaji wa kampeni ya Serikali ijulikanayo kama nyumba ni choo.

Amesema wananchi wanatakiwa kuhakikisha wanajenga vyoo bora kwa mujibu wa kanuni zote za afya hali itakayosaidia kuepuka magonjwa yakiwemo yale ya mlipuko.

Clip Afisa Afya…………………01

Akizungumzia kuhusu mapokeo ya elimu ya ujenzi wa vyoo bora kupitia kampeni ya serikali ya Nyumba ni Choo amesema shida iliyopo kila mwananchi amekuwa akiipokea kwa mtazamo wake huku kukiwa na changamoto ya namna ya kutekeleza elimu hiyo.

Clip Afisa Afya…………………02

Mmoja wa wakazi katika jijini la Dodoma ameiambia taswira ya habari kuwa ili wananchi wajenge vyoo bora ni vyema Serikali ikaendelea kutoa elimu ili kuleta hamasa kwa kiasi kikubwa.

Clip Mwananchi……………03

Serikali inahamasisha wananchi kujenga choo bora ambacho kinafuata kanuni zote tano za afya ikiwemo kuta, milango pamoja na paa.