Dodoma FM

Wakazi wa Farkwa waelimishwa juu ya uhifadhi sahihi wa mazao ya chakula

1 November 2021, 12:27 pm

Na; Selemani Kodima.

Uongozi wa kijiji cha Farakwa wilayani Chemba umesema unaendelea kutoka elimu kwa wananchi wake juu ya umuhimu wa matumizi sahihi ya chakula na uhifadhi wa mazao .

Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kijiji cha Farakwa Bw Costa Maiko ambapo amesema wameshatoa angalizo kwa wananchi wake juu ya matumizi ya nafaka katika upikaji wa pombe kutokana hali ya uzalishaji wa chakula kuwa chini kwa miaka ya hivi karibuni.

Amesema kupitia mikutano ya kijiji wamekuwa na utaratibu wa kukumbusha umuhimu wa utunzaji wa chakula na uhifadhi wa nafaka .

Kwa upande mwingine amejivunia hali ya uzalishaji wa mazao ndani ya kijiji cha farakwa ambapo amesema wananchi wake wamekuwa mstari wa mbele katika uzalishaji wa mazao ya biashara .

Amesema kuwa Msimu wa uliopita mazao ya biashara yaliofanikiwa kuzalishwa zaidi ni pamoja na ufuta ,alizeti ambayo yamekuwa muhimili wa uchumi kwa baadhi ya wakazi wa kijiji hicho.

Pamoja na hayo mwenyekiti huyo amewataka wananchi wake kuchangamkia fursa ya kulima mazao ya biashara ili kuweza kuongeza kipato.