Dodoma FM

Uzalishaji wa sukari nchini utatoa fursa kwa wakulima wa miwa na ajira kwa vijana

30 August 2021, 1:23 pm

Na;Mindi Joseph.

Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda amesema hatatoa kibali cha kuingiza sukari nchini kufuatia kuua ajira kwa watazania na kudidimiza uzalishaji wa miwa kwa wakulima Nchini.

Akizungumza leo Jijini Dodoma katika uzinduzi wa matokeo ya sensa ya kilimo mifugo na uvuvi ya mwaka 2019 /20 Waziri Mkenda amesema Hatatoa kibali ili kuwapa nafasi wakulima wa miwa kuuza miwa kutoa fursa kwa vijana kupata ajira pamoja na kuokoa fedha za kigeni.

Katika hatua nyingine prof Mkenda amesema shughuli za kilimo zimeendelea kutoa mchango katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa zaidi ya asilimia 65 na mchango wa shughuli za kilimo katika pato la taifa umeongezeka hadi asilimia 26.9 kutoka asilimia 26.6.

Naye Mtakwimu mkuu wa serikali Dkt Albina Chuwa amesema jumla ya shilingi billioni 6 zimetumika kukamilisha sensa hiyo ikilinganishwa na mwaka 2007/2008 ambapo billioni 10 zilitumika.

Sensa hiyo imekuwa ikifanyika ili kutoa takwimu sahihi za kilimo mifungo na uvuvi ambazo zitakuwa msingi wa kufuatilia na kutathimini malengo yaliyowekwa katika sera ya kilimo mifugo na uvuvi na kutayarisha sera pamoja na kufanya maamuzi sahihi katika sekta hizo.