Dodoma FM

Ushirikishwaji wa wanawake katika uzalishaji mazao waongezeka kwa asilimia 70 Dodoma

23 August 2021, 1:26 pm

Na;Mindi Joseph .


Ushirikishwaji wa wanawake katika uzalishaji wa mazao kwenye sekta ya kilimo umetajwa kuongezeka kutoka asilimia 10 hadi 70 Mkoani Dodoma.

Akizungumza na taswira ya habari afisa kilimo kata ya kigwe wilayani Bahi Bw,Dominica Sabangi Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Bahi amesema wanawake wanapewa kipaumbele kikubwa katika uzalishaji na uuzaji wa mazao tofauti na miaka mingine.

Naye Rashid Abdallah amebainisha kuwa kaya nyingi zimekuwa na desturi za kuwashirikisha wanawake katika uzalishaji wa mazao na kuchangia uchumi wa kaya kuwa imara.

Bw Abdallah Ameongeza ni wajibu wa kila kaya kuhakikisha zinashirikiana vyema kwa manufaa ya jamii na familia kwa ujumla.