Dodoma FM

Wakazi wa Mkoka waiomba serikali iwaboreshee upatikanaji wa huduma ya Afya

17 August 2021, 12:11 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Mkoka Wilaya ya Kongwa wameiomba Serikali kuwasaidia kukamilisha upatikanaji wa huduma za afya katika kituo cha afya ili kupunguza adha kwa wananchi

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa wanapata changamoto kubwa ya kusafiri kwenda hospitali ya Wilaya kufuata baadhi ya huduma ambazo hazipatikani katika kituo chao cha afya

Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoka Bw.Elia Chibago amekili kutokukamilika kwa baadhi ya huduma katika kituo chao cha afya inawalazimu wanachi kusafili umbali wa zaidi ya kilomita thelathini na tano ili kupata baadhi ya huduma hizo

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Richard Samweli amesema kuwa wanaendelea kufuatilia fedha zaidi ya milioni miatatu kwaajili ya kukamilisha baadhi ya huduma ikiwa ni pamoja na maabara, jengo la akina mama pamoja na jengo la upasuaji.

Samweli ameongeza kuwa kukosekana kwa huduma kama za uzazi katika zahanati yao zinawapa wakati mgumu wakati wa kujifungua na kuiomba Serikali kuwasaidia kukamilisha huduma hizo.

Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele katika kuboresha huduma ya mama na mtoto katika vituo vya afya mbalimbali nchini