Dodoma FM

Wazazi wametakiwa kujenga mazoea ya kuzungumzia masuala ya Afya ya uzazi na watoto wao

11 August 2021, 11:21 am

Na; Mariam Matundu.

Wazazi na walezi wametakiwa kuwa na mazoea ya kuzungumza na watoto wao kuhusu masuala ya afya ya uzazi ili kuwaepusha na magonjwa ya ngono pamoja na mimba za utotoni.

Hayo yamezungumzwa na mratibu wa afya ya uzazi jiji la Dodoma Fidea Obimbo na kuongeza kuwa kumekuwa na matukio ya mimba za utotoni yanayosababisha wanafunzi kukatisha masomo hivyo ni muhimu wakapewa elimu ya afya ya uzazi .

Aidha amesema wanaendelea kuimarisha huduma rafiki kwa vijana za kutoa elimu ya afya ya uzazi pamoja na huduma hizo ambapo pia wanawatumia waelimisha rika katika kuwafikia vijana wengi zaidi.

Taswira ya habari imezungumza na binti ambae alikatisha masomo kutokana na mimba ambapo anasema huenda angepata elimu ya afya ya uzazi kutoka kwa wazazi angeweza kutimiza ndoto zake .

Kwa upande wake maneja miradi wa taasisi ya maendelao ya vijana Dodoma DOYODO Charles Ruben amesema wamekuwa wakifanya vikao na wazazi ili kuona umuhimu wa kuzungumza na watoto wao ili kuepuka athari kwa vijana.