Dodoma FM

Wakulima wa korosho Masinyeti walalamikia upuliziaji dawa kuwa hafifu

3 August 2021, 1:55 pm

Na; Selemani Kodima.

Licha ya Serikali ya wilaya ya Kongwa kutoa kipaumbele katika kilimo cha korosho lakini inaelezwa kuwa upuliziaji wa dawa ni changamoto kwa baadhi ya wakulima katika kijiji cha Masinyeti hali inayosababisha mikorosho mingi kuduma.

Akizungumza na Taswira ya habari Afisa Mtendaji wa kijiji cha Masinyeti Ashura Elinihaki amesema Muitikio ni mkubwa kwa wakulima katika upandaji wa miche ya Korosho lakini changamoto iliyosalia ni kushindwa kuhudumia mikorosho
Amesema baadhi ya wakulima wamekuwa na dhana ya kusubiri kila jambo serikali kuwaletea hali ambayo wameshindwa kununua dawa kwa ajili ya kupulizia mikorosho kwa ajili ya wadudu.

Kwa upande mwingine amesema wamekuwa wakitumia njia ya kuendelea kuhamasisha wakulima juu ya umuhimu wa dawa katika mikorosho kupitia matangazo na Mikutano ya kijiji .

Zao la korosho katika wilaya ya Kongwa ni zao la kimkakati ambapo utekelezaji wake unalenga kuongeza kipato ,na kusaidia kurejesha hali ya uoto wa asili na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi.