Dodoma FM

Wanasayansi watakiwa kuunganisha nguvu na serikali ili kuwakomboa wakulima

23 July 2021, 12:58 pm

Na;Mindi Joseph.

Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda amesema wanasanyansi wanatakiwa kuunganisha nguvu na serikali ili kusaidia kuwakomboa wakulima nchini.

Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya pass Trust Jijini Dodoma Mh Mizengo pinda amesema kilimo ni sanyasi hivyo nguvu ya pamoja ikiunganishwa kati ya wanasanyansi na serikali itasaidia kuwakomboa wakulima wadogo ambao bado ni masikini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya pass Trust Dkt. Taus Kida,amesema kuwa sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika kukuza uchumi kwani asilimia 26.9 ya mapato ya taifa inatokana na mchango wa sekta ya kilimo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka amesema kuwa ujio wa Pass Trust utaamsha kilimo biashara Dodoma na Kanda ya Kati.

Wiki ya pass Trust inatarajia kuhitimishwa siku ya kesho ambapo waziri wa kilimo Prof Adolf Mkenda atakuwa mgeni Rasim.