Dodoma FM

Kampeni ya zero mogogoro ya ardhi Mkoani Dodoma yaongezewa siku

15 July 2021, 11:38 am

Na; Shani Nicolous.

Baada ya uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuandaa kampeni ya zero migogoro ya ardhi Mkoani Dodoma Serikali imeongeza siku ili zoezi hilo lidumu kwa muda wa mwezi mzima kwa ajili ya kuendelea kusikiliza na kutatua migogoro hiyo.

Akizungumza na Dodoma fm mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Mh. Jabiri Shekimweri amesema kuwa mwitikio umekuwa mkubwa kitu mbacho hawakutegemea, hivyo kwa kulitambua hilo wamefanya majadiliano na Mkuu wa Mkoa pamoja na wizara husika kuongeza siku ambapo itakuwa mwezi mzima na utaratibu utatolewa .

Amesema kulikuwa na migogoro zaidi ya 2300 na baadhi ya migogoro hiyo imesikilizwa huku mingine wanalazimika kufika maeneo husika ili kuona na kuitatua yakiwemo majengo na wamebaini baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa chanzo cha migogoro kutokuisha kama hati pandikizi, fidia pamoja na rushwa.

Baadhi ya wananchi Jijini hapa wameipongeza Serikali ya Mkoa wa Dodoma kwa kampeni hiyo na hatua waliyofikia kwa sasa kwani tayari kuna wanyonge wamerudisha tabasamu lao huku wakiomba mwendelezo wa utatuzi wa migogoro pamoja na elimu kuhusu namna ya kumiliki hati na ardhi kwa ujumla.

Kampeni ya ziro migogoro ya ardhi ndani ya Mkoa wa Dodoma ilikuwa ya siku 10 na ilianza July 5 hadi July 14 sasa itaendelea kwa kipindi cha mwezi mzima ndani ya mkoa wa Dodoma.