Dodoma FM

Wanaume Bahi wadaiwa kufanya unyanyasaji wa kiuchumi

12 July 2021, 1:16 pm

Na; Shani Nicolous.

Baadhi ya wanaume katika kata ya Bahi Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma wanadaiwa kufanya unyanyasaji wa kiuchumi katika familia zao hususani katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno.

Hayo yamesemwa na Diwani wa kata hiyo Bw. Agustino Ndunu wakati akizungumza na kituo hiki na amesema kata hiyo kwa sasa inakabiliwa na ukatili dhidi ya mali kwa wanawake ambapo wanaume wamekuwa wakiuza mazao ambayo yametokana na juhudu za wanandoa wote bila mawasiliano na mwenzake wao.

Amesema kwa muda mrefu kulikuwa na tabia ya wananaume kuwapiga wake zao bila sababu ambapo ukatili huo kwa sasa umepungua kutokana na vyombo mbalimbali vya habari kufuatilia vitendo hivyo pamoja na wanaharakati kupiga vita ukatili huo.

Kwa upande wake mratibu dawati la jinsia Wilaya ya Bahi amesema kuwa mila na dsturi zilizopo katika wilaya hiyo ndiyo chanzo moja wapo kinachosababisha ukatili wa vipigo na takwimu zinaonesha mwaka uliyopita hali ilivyokuwa.

Ukatili huo unatajwa kuwa chanzo cha kukosekana kwa amani kwa baadhi ya familia ambapo baadhi ya familia huvuruga muelekeo kimaisha na kusababisaha watoto kukimbia makazi yao kwa kuchoshwa na ugomvi wa kila siku kwa wanandoa.