Dodoma FM

Wakazi wa Handali waiomba serikali kuwapelekea wataalam wa uchimbaji madini.

29 June 2021, 2:09 pm

Na ;Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Handali iliyopo Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wameiomba serikali kuwapelekea wataalamu wa musuala ya madini ili kuwapatia elimu ya uchimbaji itakayo wawezesha kuchimba kwa ufanisi.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamesema uchimbaji unaenda vizuri licha ya kukosa elimu na vifaa vya kisasa huku wakiomba wawekezaji watakao wekeza wakumbuke kutatua changamoto za wananchi.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Kawawa Bw. Diksoni Muhaji amesema licha ya kuwa bado hawajapata kampuni ya moja kwa moja ya kuchimba madini lakini wanaendelea na uchimbaji wa asilimia.

Naye Diwani wa Kata ya Handali Bw.Aidani Rubeleje amesema kuwa kwa sasa tayari wawekezaji wameanza na ujenzi wa Elusion plant kwa ajili ya kuchenjua madini huku akiwakaribisha wawekezaji zaidi.

Kuna umuhimu wa kuwepo kwa majadiliano ya kisera ya haraka juu ya faida na athari za ubia na jinsi ya kuwezesha ubia huu ili kuboresha sekta ya madini na kuleta maendeleo endelevu katika jamii za uchimbaji vijijini