Dodoma FM

Elimu ya Afya ya uzazi fumbo kubwa kwa vijana wasio na uelewa

21 April 2021, 12:27 pm

Na; Mariam Matundu .

Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka vyuo mbalimbali wametajwa kuwa miongoni mwa vijana ambao bado hawana ujasiri wa kuzungumza masuala ya afya ya uzazi kwa uwazi.

Hayo yamesemwa na kijana, mwanafunzi wa chuo cha Biashara Dodoma CBE  ambae pia ni mwelimishaji rika katika masuala ya afya ya uzazi na kuongeza kuwa mara nyingi vijana hao wanakuwa waoga kuzungumza hali inayosababisha madhara makubwa kwao.

Kwa upande wake mratibu wa afya ya uzazi mama na mtoto jiji la Dodoma Fidea Obimbo amesema tatizo la vijana kutokuwa na ujasiri ni kutokana na kukosa msingi mzuri tangu wakiwa wadogo na kuwataka wazazi kuvunja ukimya na kuzungumza na watoto wao masuala ya afya ya uzazi.

Amesema kupitia elimu na taarifa za  afya ya Uzazi kwa Vijana itasaidia kupunguza mimba za ujanani , itawezesha vijana kujitunza, vilevile kuwaepusha na magonjwa mbalimbali ya zinaa.