

6 June 2023, 6:46 pm
Mradi wa ALiVE-Tanzania una lengo la kufanya tafiti na kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana Nchini.
Na Fred Cheti.
Jamii imeshauriwa kujenga desturi ya kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo yao na kubaini changamoto zilizopo ili kupunguza baadhi ya matukio yasiyofaa katika jamii ikiwemo za ukatili wa kijinsia.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Sophia Kizigo wakati akizungumza na wazazi , walezi pamoja na wanafunzi wilayani humo baada ya kuzindua mradi wa ALiVE-Tanzania wenye lengo la kufanya tafiti na kupima stadi za maisha na maadili kwa vijana nchini wenye umri kati ya miaka 13 – 17.
Kwa upande wake Bwana Johaiven Bikongolo ambae ni mkufunzi kutoka shirika hilo la ALIVE anaelezea umuhimu wa kuwa na utafiti huo.
Nao baadhi ya wazazi wilayani humo wamezungumza baada ya kupatiwa mafunzo na elimu juu ya utafiti huo unaopaswa kufanya kuanzia ngazi za familia.