Dodoma FM

Wananchi waomba maboresho soko la kimataifa Kibaigwa

30 May 2023, 4:29 pm

Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remidius Mwema akiongea na wafanyabiashara wadogowadogo wa soko ka Kimataifa Kibaigwa .Picha na Bernadetha Mwakilabi.

Soko la kimataifa la Kibaigwa ni utambulisho wa wilaya ya Kongwa kimataifa hivyo lazima litunzwe kama chanzo cha mapato.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Wafanyabiashara wadogowadogo katika soko la mazao la kimataifa la Kibaigwa wilayani Kongwa wameiomba serikali kufanya maboresho ya kisasa katika soko hilo ili kukuza biashara na kuvutia wateja wengi zaidi kutoka nje ya nchi.

Wakiongea sokoni hapo wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukosa mitambo ya kusafishia mazao ambapo kwa sasa wanatumia chekeche za mikono ambazo zimechakaa na zina mgogoro baina ya wafanyabiashara na uongozi wa soko hilo.

Sauti za wafanyabiashara

Akitolea ufafanuzi suala hilo Afisa Biashara wa soko hilo Bwana Luig Mbuya amesema kuwa uongozi wa soko na wafanyabiashara walikubaliana kuwa chekeche hizo zinunuliwe na kugawiwa Kwa makundi ya wafanyabiashara na endapo zitachakaa basi wanakikundi watazirekebisha, suala ambalo wafanyabiashara hao hawakutekeleza.

Sauti ya Afisa Biashara wa soko hilo.

Aidha mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel amesema kupitia Hali hiyo Kuna haja ya uongozi wa soko kukutana mara Kwa mara na wafanyabiashara hao ili kujua changamoto zao na kuzitatua mapema.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.

Hata hivyo Mwema ameonesha kutoridhishwa na mchakato wa usafishaji mazao sokoni hapo na kuongeza kuwa Soko la kimataifa la Kibaigwa ni utambulisho wa wilaya ya Kongwa kimataifa hivyo lazima litunzwe kama chanzo Cha mapato.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
 Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remidius Mwema ,kamati ya ulinzi na usalama, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Kongwa na wataalam mbalimbali walipotembelea soko la mazao la kimataifa Kibaigwa kujionea hali ya soko. picha na Bernadetha Mwakilabi.

Kwa upande wake Kaimu meneja wa soko la kimataifa la Kibaigwa Bwana Athman Nzenga amekili kuwepo kwa changamoto za uchakavu wa miundombinu ikiwemo mitambo ya kusafishia mazao, ukosefu wa uzio na Kamera za ulinzi zitakazosaidia kudhibiti upotevu wa mapato.

Hata hivyo Nzenga ameongeza kuwa Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mapato ya soko hilo yalikuwa milioni 900 na mwaka 2022/2023 mwezi machi yalikuwa milioni 928 na kwamba mapato yanaongezeka mwezi June Hadi disemba msimu wa mavuno ya mazao ya mahindi alizeti Karanga na mbaazi.

 Mkuu wa wilaya ya Kongwa Remidius Mwema ,kamati ya ulinzi na usalama, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Kongwa na wataalam mbalimbali walipotembelea soko la mazao la kimataifa Kibaigwa kujionea hali ya soko. picha na Bernadetha Mwakilabi.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya Kongwa Bwana Fortunatus Mabula amesema kuwa ofisi ya Mkurugenzi ina taarifa ya changamoto hizo na ipo kwenye hatua za utekelezaji.