Dodoma FM

Wananchi watakiwa kutumia mabwawa yanayojengwa kujikita katika kilimo cha umwagiliaji

19 May 2023, 7:36 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule akiwa na viongozi mbalimbali akikagua bwawa la Kongogo linalotarajia kujengwa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji. Picha na Mariam Kasawa.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma imefanyika wilayani Bahi lengo likiwa ni kutembelea miradi mbalimbali wilayani humo ikiwemo ujenzi wa shule ya msingi Ngondo, nyumba ya mwalimu na mradi wa umwagiliaji Kongogo.

Na Mariam Kasawa.

Wananchi wametakiwa kutumia vizuri mabwawa yanayo jengwa kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji ili waweze kuachana na kilimo cha kubahatisha.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule alipo kuwa akizungumza na wakazi wa kata ya Babayu kijiji cha Kongogo wilayani Bahi alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani humo.

Bi Senyamule amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanaachana na kilimo cha kubahatisha na kujikita katika kilimo cha umwagiliaji .

Sauti ya Mkuu wa Mkoa.
Wakazi wa Kongogo wakiwa katika Mkutano. Picha na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Mkoa alitoa nafasi kwa wananchi wa kata hiyo kutoa kero zao mbalimbali ambazo zilipatiwa majibu na wataalamu.

Sauti za Wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa wialaya ya Bahi Mh. Godwin Gondwe akisoma taarifa ya kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amesema wamejiwekea mkakati wa kukamilisha miradi mapema .