Dodoma FM

Hospitali ya Benjamini Mkapa yazindua huduma ya upandikizaji Uloto

10 May 2023, 8:01 pm

Waziri mkuu wa Tanzania mh. Khassim Majaliwa akizungumza katika uzinduzi huo. Picha na Noah Patrick.

Nchi ya Tanzania inashika nafasi ya 4 kuwa na wangojwa wengi ulimwenguni wa Selimundu huku wenye watoto Elfu 11000 kwa mwaka wanaweza kufa kabla ya kufikisha umri wa miaka 5  sawa na asilimia 50 hadi 90.

Na Mariam Kasawa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali iliamua kuwekeza shilingi bilioni 2.7 ili kuanzisha huduma ya upandikizaji uloto na kupunguza gharama za matibabu hayo kwa wananchi.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo  Leo katika Uzinduzi wa Huduma za upandikizaji uloto katika Hospital ya Benjamin Mkapa na ameitaka Wizara ya afya kuendela kuhakikisha Watoto wachanga wanaozaliwa wanapimwa ugonjwa wa selimudu.

Sauti ya Waziri mkuu .

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amewataka Wazazi wenye watoto wenye ugonjwa wa selimundu kwenda kwa wataalamu.

Sauti ya waziri wa Afya.

Tayari huduma ya upandikizaji uloto imefanyika kwa watoto 3 wenye ugonjwa selimundu na hapa Watoto na wazazi Wanatoa ushuhuda.

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi katika uzinduzi huo uliofanyika katika hospitali ya Benjamini Mkapa. Picha na Noah Patrick.

Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali ya Benjamin Mkapa, Dkt. Alphonce Chandika anasema upandikizaji wa Uloto  umefanyika kwa mara ya kwanza Tanzania na kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa Nchi 7 zinazotoa huduma hii.

Sauti ya Dkt Chandika.