Dodoma FM

Wakazi wa Msalato waomba mazingira ya mnada kuboreshwa

2 May 2023, 3:49 pm

Picha ni muonekano wa mnada wa Msalato sehemu ambapo yapo majiko ya kuchomea nyama.Picha na Thadei Tesha.

Mnada wa nyama msalato ni miongoni ma maeneo maarufu ya asili ambapo wananchi hufika kwa ajili ya kujipatia nyama choma .

Na Thadei Tesha.

Wakazi wa Msalato Jijini Dodoma wameiomba serikali  kuboresha mazingira ya  eneo la mnada wa msalato ambao ni maarufu kwa kuuza nyama choma siku ya jumamosi.

Dodoma Tv imefika katika eneo ulipo mnada huo na kuzungumza na baadhi ya wananchi wa eneo hilo ambapo wanasema kuwa pamoja na eneo hilo kutoa fursa kwa vijana lakini mazingira ya eneo hilo si ya kuridhisha.

Sauti za wakazi wa Msalato
Picha ni takataka zilizo rundikwa karibu na eneo hilo la mnada wa Msalato ambazo gari hupita kukusanya.Picha na Thadei Tesha.

Mwenyekiti wa eneo hilo anesema kuwa pamoja na kuwa mnada huo unachangia kwa kiasi kikubwa katika suala la kutoa fursa kwa vijana na watu kujipatia nyama choma siku ya jumamosi lakini wameendelea kutuma maombi kwa mkurugenzi wa jiji kwa ajili ya kuboresha eneo hilo .

Sauti ya Mwenyekiti wa eneo hilo.