Dodoma FM

BOOST kuboresha elimu kongwa

19 April 2023, 2:20 pm

Baadhi ya wanakamati ya usimamizi wa mradi wa BOOST wakiwa katika kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo .Picha na Halmashauri ya wialaya ya Kongwa.

Mradi wa BOOST ulianzishwa na Serikali chini ya ufadhili wa benki ya dunia unaosimamiwa na ofisi ya Rais TAMISEMI  utatumia zaidi ya bilioni 1 na milioni 352 kutekeleza ujenzi huo ambao ni moja ya afua zake.

Na Bernadetha Mwakilabi.

Mradi wa BOOST unatarajia kujenga shule mpya mbili vyumba vya madarasa vilivyokamilika 26  vyoo 18 na darasa la elimu maalum moja katika shule za msingi na awali wilayani Kongwa.

Hayo yameelezwa na Mwalimu Magreth Temu Afisa Elimu Awali na Msingi wilaya ya Kongwa wakati akielezea kwa ufupi taarifa ya maandalizi ya utekelezaji wa ujenzi kupitia mradi wa BOOST ambapo amesema ujenzi huo utafanywa katika shule za msingi 9 za wilayani humo zikiwemo Ihanda juu, Mtanana, Tubugwe, Wangazi na shule mpya ya Moleti.

Sauti ya Afisa Elimu Awali na Msingi wilaya ya Kongwa.

Akipokea taarifa hiyo mbele ya wajumbe wakiwemo kamati ya ulinzi na usalama Mkuu wa wilaya ya Kongwa Mheshimiwa Remidius Mwema Emmanuel amesisitiza kazi zote za ujenzi zifanywe na mafundi wazawa na vifaa vyote vya ujenzi vinunuliwe kwa wafanyabiashara wazawa wakazi wa Kongwa ili kukuza uchumi wa wananchi wake.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.
Mwalimu Magreth Temu Afisa Elimu Awali na Msingi wilaya ya Kongwa. Picha na Halmashauri ya wilaya ya Kongwa.

Aidha Mwema ameongeza kuwa viongozi wanatakiwa kushirikisha wananchi katika ujenzi wa miundombinu hiyo na miradi mingine ya maendeleo kwani nguvu za wananchi ni sehemu ya kutekeleza miradi.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kongwa Dkt. Omary Nkullo. Picha na Halmashauri ya wialaya ya Kongwa.

Sambamba na hayo nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kongwa Dkt. Omary Nkullo ametilia mkazo suala la ushirikishwaji uwazi na ukweli juu ya taarifa za ujenzi wa miundombinu hiyo ili kuondoa mashaka kwa wananchi.

Sauti ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Kongwa Dokta Omary Nkullo