Dodoma FM

Tishio la upungufu wa Chakula Dodoma

31 March 2023, 6:50 pm

Muonekano wa mazao katika moja ya shamba jijini Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Upungufu wa mvua umepelekea mazao yaliyopandwa kushindwa kuvunwa kama matarajio ya Mkoa yalivyokuwa.

Na Mindi Joseph.

Mkoa wa Dodoma unakabiliwa na tishio la kupata upungufu wa chakula kwenye baadhi ya maeneo kutokana na mvua zilizotarajiwa kwa msimu huu kunyesha chini ya wastani.

Hayo yamebainishwa leo wakati wa kikao cha wadau wa kilimo wa Halmashauri zote nane za Mkoa wa Dodoma kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Rosemary Senyamule kujadili namna ya kukabiliana na tishio la njaa ambalo linaweza kuukumba Mkoa endapo suluhisho la haraka halitafanyika.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma
Muonekano wa mazao katika moja ya shamba jijini Dodoma. Picha na Mindi Joseph.

Kufuatia hali hii, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewagiza Wakuu wa Wilaya kusimamia kila Halmashauri na kuweka mkakati wa namna ya kukabiliana na tishio la upungufu wa chakula na kuchukua tahadhari kabla ya shari.

Senyamule ametoa rai kwa wakazi wa Dodoma kujifunza namna ya kuweka akiba ya chakula na kutafuta suluhisho la kudumu kama Mkoa.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Mkoa wa Dodoma ulijiwekea malengo ya kulima hekta 7 za chakula lakini mvua hazikunyesha kama ilivyotarajiwa hivyo kuathiri upatikanaji wa chakula kama ilivyotarajiwa kuilazimu Serikali kutoa mahindi ya bei nafuu jumla ya tani 12,747.15.