Dodoma FM

Wananchi watakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya Marburg

22 March 2023, 6:26 pm

Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akizungumza na vyombo vya habari.Picha na Wizara ya Afya

Ugonjwa huu huambukizwa kutoka kwa Binadamu mmoja kwa mwingine hususani kwa njia ya kugusa majimaji ambayo yanaweza kuwa mate , mkojo, damu, machozi au kinyesi yatokayo kwenye maiti au Mgonjwa mwenye dalili, maambukizi pia yanaweza kutoka kwa Wanyama kwenda kwa Binadamu iwapo Mtu atakula au kugusa mizoga au Wanyama walioambukizwa”

Na Mariam Kasawa.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema uchunguzi wa Maabara ya Taifa umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg katika Mkoa wa Kagera ambavyo vinasababisha ugonjwa wa Marburg Virus Disease (MVD).

Ugonjwa huo hadi sasa umesababisha vifo vya Watu watano ambapo Ugonjwa huo hauna tiba mahususi bali hutibiwa kwa dalili anazokuwa nazo Mgonjwa.

Akizungumza  leo jijini Dar es salaam, Waziri Ummy amesema uchunguzi ambao umefanywa katika Maabara  ya Taifa ya Afya ya Jamii umethibitisha uwepo wa virusi vya Marburg ambavyo vinasababisha ugonjwa unaojulikana kama Marburg Virus Disease(MVD)”

Sauti ya Waziri wa Afya.

Akitaja dalili za ugonjwa huo Waziri ummy amesema.

Sauti ya Waziri wa Afya.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa mapema katika vituo vya Afya vilivyo karibu pindi wanapo ona au kuona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo.

Sauti ya Waziri wa Afya.

Itakumbukwa siku tano zilizopita Serikali kupitia Wizara ya Afya ilitoa tahadhari juu ya uwepo wa ugonjwa ambao bado ulikuwa haujajulikana Mkoani Kagera katika Wilaya ya Bukoba Vijijini ambapo Watu 7 walisadikika kupata dalili za homa, kutapika, kutokwa damu maeneo mbalimbali ya mwili na figo kushindwa kufanya kazi na Watu watano kati yao wakaripotiwa kufariki.