Dodoma FM

TPF Net kuendeleza kudhibiti na kutokomeza vitendo vya ukatili

9 March 2023, 12:00 pm

Jeshi la Polisi nchini kupitia Mtandao wa polisi wanawake nchini TPF Net.Picha na Martha Mgaya

TPF Net limesema limejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali katika kudhibiti na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Na Fredi Cheti.

Jeshi la Polisi nchini kupitia Mtandao wa polisi wanawake nchini TPF Net limesema limejipanga kushirikiana na wadau mbalimbali katika kudhibiti na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, Suzana Kaganda.Picha na Martha Mgaya

Kauli hiyo imetolewa na kamishna wa Utawala na Rasilimali Watu, Suzana Kaganda katika maadhimisho ya siku ya wanawake dunia yaliyoandaliwa na jeshi hilo kupitia mtandao huo wa polisi wanawake nchini.

Sauti ya Suzana Kaganda.

Aidha Kmanda Kagundu ameelezea mikakati ya jeshi hilo katika kuhakikisha linakomesha vitendo vya ukatili kwa jamii huku akiwataka pia wanaume wanaofanyiwa ukatili kufika katika vyombo vya sheria.

Sauti ya Suzana Kaganda.

Kila mwaka Machi 08, Umoja wa Mataifa husheherekea haki zilizopatikana kwa bidii za wanawake na kuangazia changamoto ambazo bado ziko mbele katika kukomesha ubaguzi wa kijinsia katika karibu nyanja zote za maisha.