Dodoma FM

Mpwapwa yatarajia kuanza  kilimo cha umwagiliaji

6 March 2023, 11:40 am

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma mh. Rosemary Senyamule akikagua ujenzi wa bwawa wilayani Mpwapwa. Picha na Mariam Kasawa.

Bwawa hilo ambalo linajengwa kati ya kijiji cha Chunyu na Ng’ambi wilayani Mpwapwa hadi sasa umefikia asilimia 30 huku ukitarajiwa kukamilika ifikapo Novemba mwaka huu.

Na Mariam Kasawa

Jumla ya shilingi bilioni 27 zimetolewa ili kukamilisha uchimbaji wa bwawa litakalo tumika kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji katika Wilaya ya Mpwapwa.

Akizungumza katika ziara ya kuutembelea mradi huo  mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi. Sophia Kizigo ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akisema tayari wamekwisha anza kuwaandaa wananchi kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi. Sophia Kizigo

Akiongea kabla ya kumkaribisha kiongozi wa ziara mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemery Senyamule katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga amesema bwawa hilo linatakiwa kutumika kwa ajili ya kuongeza uchumi wa mkoa wa dodoma.

Sauti yakatibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatma Mganga.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemery Senyamule akizungumza katika  ziara hiyo amesisitiza ujenzi wa bwawa hilo linalounganisha kata mbili ufanyike kwa ubora na kwa wakati.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemery Senyamule

Mkandarasi wa ujenzi huo  Eng Nuru Simkoko amesema muda wa utekelezaji wa mradi huo ni miezi 12 hadi kukamilika kwake.