Dodoma FM

UWT Bahi walipongeza  Dawati la Jinsia na Watoto

3 March 2023, 2:50 pm

Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) . Picha na Benard Magawa.

Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za ukatili ili kumsaidia kila mmoja kuishi kwa furaha .

Na Bernad Magawa

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunuani ambayo hufanyika machi  8 kila mwaka, Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT)  Wilaya ya Bahi Wametebelea dawaji la jinsia na watoto Wilaya ya Bahi kujionea huduma zinavyotolewa.

Ziara hiyo iliyohusisha viongozi  na Baadhi ya wanachama  wa Jumuiya hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa UWT  Wilaya ya Bahi Imakulata Masigati imefanyika  Machi 3,2023  kama sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika kimkoa  wilaya ya Kondoa.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Imakulata ameeleza kufurahishwa na namna wanawake wilayani Bahi wanavyo hudumiwa katika kitengo hicho ambacho kinahusika na ukatili mbalimbali  wa jinsia na watoto katika jamii huku akitoa rai kwa wananchi hususa ni wanawake kulitumia dawati hilo kutatua changamoto mbalimbali walizonazo.

“Nimefurahishwa na utendaji kazi wa Dawati, wanafanya kazi vizuri, ni wakarimu na wanasikiliza kwa makini bila ukali, hivi ndivyo huduma nyeti kama hii zinavyopaswa kutolewa kwa wananchi hasa wenye matatito kama haya ya unyanyasaji wa jinsia na watoto.” Amesema Masigati

Sauti ya Mwenyekiti wa UWT  Wilaya ya Bahi Imakulata Masigati.

Naye katibu wa Jumuiya hiyo Hilda Mdaki akizungumza  katika ziara hiyo amewapongeza dawati la jinsia Wilaya ya Bahi kwa utendaji  kazi mzuri  na kueleza kuwa Watumishi wamekuwa wakiwahudumia wananchi  kwa ukarimu mkubwa.

Sauti ya katibu ya katibu wa Jumuiya Hilda Mdaki .

Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto wilaya ya Bahi Mkaguzi wa Polisi Edison Kaitaba amesema kwa kiasi kikubwa wanawake ndiyo wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kupata huduma katika dawati hilo kuliko wanaume na kueleza changamoto zinazowakabili huku kubwa ikiwa ni jamii kuficha taarifa za ukatili unaotokea katika jamii wanazoishi.

Sauti ya Mkuu wa Dawati la Jinsia na watoto wilaya ya Bahi Mkaguzi wa Polisi Edison Kaitaba.

Mkuu huyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za ukatili ili kumsaidia kila mmoja kuishi kwa furaha na kusema kuwa unapotoa taarifa fiche kuhusiana na ukatili dawati lina utaratibu mzuri wa kumlinda mtoa taarifa asijulikane popote hivyo wananchi wasiogope kutoa ushirikiano kwa Polisi wa Dawati la Jinsia.