Dodoma FM

Wanafunzi watembea zaidi ya kilomita 28 kufuata shule

28 February 2023, 5:21 pm

Picha ya wanafunzi . picha na Tanzania home page.

Serikali imeombwa kusaidia kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari ili kurahisha upatikanaji shule hali itakayopunguza gharama kwa wazazi wanaosomesha watoto .

Na Victor Chigwada                                                       

Wanafunzi wa kata ya chiboli wilayani chamwino wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya km 28 kila siku kwaajili ya kwenda shule ya sekondari Fufu.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa kijiji  cha  Champumba Bw.John Mdabaji  ambapo amesema kuwa kutokana na adha ya umbali huo wamejaribu kujenga baadhi ya vyumba vya madarasa ambavyo bado havijakamilika kwa kutumia nguvu za wananchi

sauti ya Mwenyekiti wa kijiji  cha  Champumba Bw.John Mdabaji.

Naye Diwani wa Kata ya Chiboli Bw.Wiliamu Teu amesema kuwa wameendelea na juhudi za ujenzi wa sekondari  na  kuwaomba wadau pamoja na Serikali kuwasaidia kukamilisha ujenzi huo

Sauti ya Diwani wa Kata ya Chiboli Bw.Wiliamu Teu

Teu ameongeza kuwa changamoto ya kilomita 28 za kufuata elimu ya sekondari imekuwa ikiongeza gharama za kimaisha kwa wazazi hususani wale wa hali ya chini

Sauti ya Diwani wa Kata ya Chiboli Bw.Wiliamu Teu