Dodoma FM

Vyombo vya habari vyatakiwa kutoa elimu

27 February 2023, 4:16 pm

Wito huo Umetolewa leo jijini Dodoma na Mhandisi David Pallangyo Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira.Picha na Maelezo

Wito kwa vyombo vya habari nchini kutumia nguvu iliyonayo katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo mbalimbali vya maji.

Na Mindi Joseph.

Wito umetolewa kwa vyombo vya habari nchini kutumia nguvu iliyonayo katika kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo mbalimbali vya maji ili kuvilinda kwa matumizi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Wito huo Umetolewa leo jijini Dodoma na Mhandisi David Pallangyo Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira Mkoani Iringa (IRUWASA) wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini hapa juu utekelezaji wa mambo mbalimbali unaofanywa na mamlaka hiyo katika mkoa huo ambapo amesema tatizo la uharibu wa vyanzo vya maji ni la nchi nzima.

Sauti ya David Pallangyo Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira.

Aidha Bwana ametoa wito kwa mamalka nyingine za Maji katika mikoa mingine ambazo haziajaanza kutumia mita za Pre-Paid kuanza kufanya hivyo kwa kuwa mita hizo zinatoa imani kwa mwananchi kulipia anachokitumia.

Sauti ya David Pallangyo Mtendaji mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa mazingira.