Dodoma FM

Wanufaika wa mpango wa TASAF Bahi wameishukuru serikali

21 February 2023, 3:32 pm

Wanufaika wa mpango wa TASAF katika kijiji cha Bahi Sokoni wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma.Picha na Bernad Magawa

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka mpango maalumu wa kusaidia kaya masikini ambao utaleta ahueni.

Na Bernad Magawa.

Wanufaika wa mpango wa TASAF katika kijiji cha Bahi Sokoni wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma wameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweka mpango maalumu wa kusaidia kaya masikini ambao umeleta ahueni kwa kaya hizo ambazo zilikuwa katika hali ngumu ya kimaisha.

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa kijiji cha Bahi Sokoni Sifaeli Mbeti pamoja na wananchi katika mkutano na wanufaika wa mpango huo ukiofanyika februali 21, 2023 katika ofisi ya kijiji cha Bahi sokoni.

Hayo yamesema na Mwenyekiti wa kijiji cha Bahi Sokoni Sifaeli Mbeti.

“Jumla ya kaya zinazonufaika na mpango wa kusaidia kaya masikini katika kijiji cha Bahi sokoni ni 383 zenye watu mchanganyiko.”

“Jumla ya kaya zinazonufaika na mpango wa kusaidia kaya masikini katika kijiji cha Bahi sokoni ni 383 zenye watu mchanganyiko wakiwemo wanawake na wanaume, mpango huu umesaidia sana upatikanaji wa chakula katika kaya hizo ukilinganisha na ugumu wa hali ya mwaka huu hivyo tunaishukuru serikali kwa mpango huu.” Amesema Mbeti.

Mwenyekiti wa kijiji cha Bahi Sokoni Sifaeli Mbeti.

Amesema mpango huo umesaidia familia ambazo hapo awali hazikuwa na uwezo wa kujihudumia kwa kuwapa mahitaji muhimu watoto wanaosoma na kupata mahitaji mengine muhimu katika familia.

Wananchi wanaonufaika na mpango wa TASAF mameeleza shukranizao kwa serikali kwa upendo wake kwa watanzania wa hali ya chini kwa kuwaletea mpango ambao umekuwa mkombozi kwao.

Sauti ya Santina.

“Tunamshukuru Rais wa Tanzania mama Samia Suluhu Hasan kwakutuwezesha kaya masikini kupitia mpango huu wa TASAF, kwa sasa tunaweza kupata milo mitatu, tuna biashara ndogondogo, na tunaweza kufuga mifugo midogo midogo kama bata, kuku, mbuzi na pia tunaweza kugharamia mahitaji ya watoto wa shule.”

Sauti ya Leonard Shaji.

Kaya hizo ambazo zinapokea mafao ya kati ya shilingi elfu 24 ikiwa ni kiwango cha chini mpaka shilingi 176 elfu ikiwa ni awamu ya pili huku wakisubiri awamu ya tatu nay a nne zimeelezwa kuwa na mabadiliko makubwa kimaendeleo ukilinganisha na hali zao hapo awali kabla ya kuingia katika mpango huo.