Dodoma FM

Ukosefu wa nishati ya umeme yaleta chuki kwa viongozi

8 February 2023, 12:50 pm

Kukosekana kwa huduma ya nishati ya umeme kwa baadhi ya vitongoji katika Kata ya Idifu.Picha na Nishati

Imelezwa kuwa kukosekana kwa huduma ya nishati ya umeme kwa baadhi ya vitongoji katika Kata ya Idifu imesababisha baadhi wananchi kujenga chuki kwa viongozi na kutaja kitendo cha kukosekana kwa nishati hiyo ni uzembe wa viongozi.

Na Victor Chigwada.

Mwenyekiti wa kijiji cha Idifu Bw. Atanasio Mgonhwa akijibia Malalamiko ya wananchi juu ya changamoto hiyo , na hapa ananza kwa kuelezea adha wanayopitia kutokana mzigo wa lawama wanaobebeshwa na wananchi kuhusu Umeme kijiji hapo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Idifu Bw. Atanasio Mgonhwa .

Mgonhwa amesema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwashushia heshima viongozi wa vijiji na kata ya Idifu kwa ujumla licha ya utekelezaji mzuri wa miradi mbalimbali ya umeme.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Idifu Samweli Kaweya amesema kuwa baadhi maeneo yamefanikiwa kufikiwa na huduma umeme ndani ya kata hiyo na tayari wamesha orodhesha majina ya vitongoji vyenye uhitaji wa huduma hiyo.

Diwani wa Kata ya Idifu Samweli Kaweya.