Dodoma FM

Wizara ya Afya yaja na mkakati wa kuzuia magonjwa yasiyopewa kipaumbele

1 September 2022, 8:39 am

Na ;Benard Filbert .

Wizara ya afya imesema kuwa imekuja na mpango wa taifa wakudhibiti magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele lengo likiwa  kumezesha dawa za kinga tiba katika ngazi ya jamii.

Hayo yanajiri kutokana na  baadhi ya magonjwa kutokupewa kipaumbele licha ya athari ambazo zinaonekana  za magonjwa hayo.

George Kabona ni mratibu wa taifa wa mpango wa kudhibiti magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele kutoka wizara ya afya amesema mpango huo unagusa kila sehemu lengo  ni kuondoa magonjwa hayo.

.

Akitaja mpango huo amesema ni kwa ajili ya magonjwa matano ambayo ni Kichocho,Minyoo ya Tumbo,Trakoma,Matende/Busha pamoja na Usubi.

.

Wizara ya afya kupitia Mpango wa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kiupaumbele imedhamiria kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwa ikiikumba jamii.