Dodoma FM

Wanawake watakiwa kutambua nafasi yao katika kuchangia maendeleo ya familia

19 July 2022, 1:59 pm

Na; Victor Chigwada.

Afisa maendeleo ya jamii katika Kata ya Msamaro Bi.Ngw’ashi Mhuli ametoa wito kwa wanawake kutambua kuwa wananafasi ya kuchangia maendeleo katika ngazi ya familia mpaka ngazi ya taifa

Bi. Mhuli akizungumza na taswira ya habari amesema kuwa uwepo wa Rais mama Samia Suluhu Hassani itaongeza chachu kwa wanawake kuwa na ujasiri  wa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo

.

Aidha Bi. Mhuli ameongeza kuwa nafasi ya Rais Samia itafungua akiri na maono kwa mwanamke na kuwabadilisha mtazamo na kujiona ni watu wanaoweza kuleta mabadiliko kwani baadhi ya wanawake hujifunza kwa wanawake wenzao waliopiga hatua kimaendeleo

.

Nao baadhi ya wananchi wamekiri na kueeleza jinsi ambavyo mwanamke ana nafasi katika jamii ili kuchangia maendeleo na suala la kuongoza tofauti na awali ambapo ilionekana mwanamke hawezi kufanya chochote

 

.

Kwa kipindi cha sasa wanawake wengi wamekuwa wakipewa nafasi kubwa za kuongoza katika taasisi za serikali na zisizo za kiserikali na wameonesha uwezo mkubwa hususani kwenye kuchagiza maendeleo kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa