Dodoma FM

Wakazi wa Mlowa bwawani wapata huduma ya maji safi na salama

11 July 2022, 2:02 pm

Na;Mindi Joseph .

Imeelezwa kuwa kukamilika kwa ujenzi wa tenki la maji linalojengwa Mlowa Bwawani litasaidia wananchi kupata maji safi na salama na kuondokana na kutumia maji ya chumvi.

Taswira ya habari imezungumza na Diwani wa kata hiyo Andrew Richard ambapo amesema wanachi wake wamekuwa wakitumia maji ambayo si safi na salama.

Ameongeza kuwa ujenzi wa Tenki hilo utakapokamilika utasaidia kuondoa adha hiyo.

.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuwa na subira kwani serikali inafanya jitihada za kuhakikisha wanapata maji safi na salama.

.

Kukamilika kwa kwa tenki italeta ahueni kwa wananchi kupata maji safi na salama na kuondokana na changamaoto  wanayokumbana nayo kwa sasa .