Dodoma FM

Chigongwe walalamikia ukosefu wa nyumba za walimu

28 June 2022, 8:43 am

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa Kata ya Chigongwe jijini Dodoma wamelalamikia ukosefu wa nyumba za walimu pamoja idadi ndogo ya walimu katika shule ya msingi Ngh’ambala.

Baadhi ya wananchi hao wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuwa changamoto ni idadi kubwa ya wanafunzi ambayo haienani na idadi ya walimu walioopo ambao nao hawana nyumba za kuishi.

.

Mwenyekiti wa mta wa Ngh’ambala  Bw.Wiliamu Nado amekiri shule hiyo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu pamoja na nyumba zao hata hivyo uchakavu wa majengo ukiwa ni adha nyingine

.

Naye Diwani wa Kata hiyo Bw.Simoni Machela amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo licha ya kuendelea na hamasa kwa wanachi kujenga baadhi vyumba ili kuwapunguzia umbali mrefu kwa baadhi ya wanafunzi

.

Mazingira ya kufundishia mashuleni ikiwa ni pamoja na walimu,nyumba za walimu na vyumba vya madarasa imekuwa chachu ya ufaulu kwa wanafunzi