Dodoma FM

Wakazi wa mgodi wa Nholi waomba kupatiwa huduma za kijamii

23 June 2022, 2:43 pm

Na; Victor Chigwada.

Kukosekana kwa huduma za kijamii katika maeneo ya migodini kumekuwa kukisababisha changamoto mbalimbali licha ya migodi kuwa chanzo cha mapato kwa serikali.

Mkemia mkuu wa mgodi mwa Nholi Bw.Renatusi Lukumila amekiri kuwa mgodi wa Nholi bado miongoni mwa migodi inayokosa huduma za kijamii Kama vile zahanati na shule licha ya idadi kubwa ya wakazi wanao lizunguka eneo hilo.

.

Bw.Lukumila ameongeza kuwa licha ya uzalishaji mkubwa uliopo mgodini hapo lakini wamekosa huduma ya ulinzi wa kujitosholeza kwani hakuna kituo Cha polisi na kupelekea watu kuishi kwa mashaka

.

Hata hivyo Halmashauri kwa kushirikiana na ofisi za mkuu wa wilaya zinajukumu la kuboresha sehemu mbalimbali Zinazo ingiza mapato Serikalini hususani maaneo ya migodini ambako ndiko huzalishwa fedha nyingi.