Dodoma FM

Tume ya umwagiliaji yatakiwa kujenga mfumo imara wa skimu za umwagiliaji

17 May 2022, 2:34 pm

Na;Mindi Joseph.

Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe ameitaka Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kujenga mfumo imara wa kusimamia Skimu za Umwagiliaji nchini.

Akizungumza Jijini Dodoma katika katika kikao kazi cha Menejimenti na Wakandarasi amesema kipaumbele cha Wizara yake katika Mwaka wa fedha 2022- 2023 ni Umwagiliaji.

Mheshimiwa Bashe amesema Tume ihakikishe asilimia 50% ya bidhaa zitokanazo na mazao zinazalishwa nchini kupitia kilimo cha Umwagiliji ifikapo mwaka 2030 .

.

Kwa upande wake Mkandarasi Patric Swai amesema katika ujenzi wa miradi wanakumbana na changamoto na ameshukuru waziri kwa kuwaunganisha na wabunge wa maeneo ambayo miradi hiyo inatekelezwa.

.

Aidha amesisitiza  Menejimenti pamoja na watumishi wa  Tume ya Taifa ya Umwagiliaji  kufanya kazi kwa bidii, weledi, ikiwemo  muda wa ziada ili kufanikisha malengo yaliyowekwa na Serikali kufikia Hekta Milioni Moja laki mbili Mwaka 2025.