Dodoma FM

Mkoa wa Dodoma kuendelea kusaidia watoto wanao ishi katika mazingira magumu

5 May 2022, 2:11 pm

Na;Mindi Joseph.

Mkoa wa Dodoma umesema utaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira Magumu na hatarisha kwa kuhakikisha wanapata mahitaji muhimu.

Taswira ya habari imezungumza na Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Dodoma Bi Honoratha Rwegasira amesema uwepo wa Baraza la watoto wanaoishi katika mazingira magumu itakuwa rahisi kuwafikia watoto hao.

Ameongeza kuwa Baraza la watoto lina tija kubwa kwani halitawabagua watoto hao katika maeneo mbalimbali.

.

Katika hatua nyingine amesema jukwaa hili litawakutanisha watoto na kujadili changamoto zao na kuzifikisha sehemu husika.

.

Aidha jitihada za pamoja zinahitajika ili kuendelea kuwasaidia Watoto wanaoisha katika mazingira magumu