Dodoma FM

Wafanyakazi wa Majumbani waomba serikali kutengeneza sera na miongozo

2 May 2022, 3:11 pm

Na;Mindi Joseph .

Wafanyakazi za Ndani wameomba serikali kutengeneza sera na miongozo itakayowasaidia kuwalinda na unyanyasaji na ukatili wa kijinsia pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wafanyakazi za ndani ambapo wamesema changamoto wanazokumbana nazo ni unyanyasaji licha ya kuwa na jukumu kubwa la kulea watoto.

Wameongeza kuwa endapo serikali itaweka sera itawasaidia kuwalinda na ukatili unaowakabili wawapo kazini

.

Katika hatua nyingine Taswaira ya habari imezungumza na mwanasheria Gidius Kato Mratibu wa programu ya mlinzi wa Haki chini ya kituo cha sheria na haki za biandamu amesema  changamoto hizi sheria inashindwa kuzitatua kutokana na kutokuwa na mikataba rasmi.

.

Aidha amesema kuwa watunga sera wana jukumu la kuhakikisha kunawepo na sera au sheria itakayowalinda wafanyakazi wa ndani.