Dodoma FM

Uvutaji wa sigara hadharani upigwe marufuku

5 April 2022, 1:37 pm

Na;Yussuph Hassan.

Wananchi Jijini Dodoma wameiomba Serikali kutilia mkazo suala la baadhi ya watu kuvuta sigara hadharani kwani suala hilo limekuwa na madhara makubwa kiafya.

Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya wakazi hao wamesema kuwa kutokana na baadhi ya watumiaji wa sigara kuvuta katika mikusanyiko ya watu yawezekana Dhahiri ikawa wanafahamu au kutofahamu madhara ya kufanya hivyo.

Nao baadhi ya watumiaji wa bidhaa hiyo wamesema inawawia vigumu kuacha kutumia bidhaa hiyo kutokana mazingira pamoja na urahibu walio nao.

Suala la uvutaji wa sigara ni suala nyeti ambapo kwa miaka kadhaa wanaharakati na wataalamu wa afya wamekuwa wakipinga vitendo hivyo kutokana na athari zake kiafya kwa mtumiaji.

Uvutaji wa sigara katika maeneo ya mikusanyiko umekuwa na madhara makubwa kiafya kwa watu waliopo eneno husika, Sigara imekuwa na watumiaji wa makundi ya watu wa aina mbalimbali huku kila mtu akiwa na hisia zake pindi anapotumia bidhaa hiyo.