Dodoma FM

Watoto wenye upungufu wa damu na maumivi ya viungo wametakiwa kupelekwa hospitali mara kwa mara

28 March 2022, 2:30 pm

Na;Yussuph Hassan.                                            

Wito umetolewa kwa Wazazi na Walezi Jijini Dodoma kuwapeleka vituo vya afya watoto wenye upungufu wa damu na maumivu ya viungo mara kwa mara, kwani inawezekana ikawa moja wapo ya dalili ya ugonjwa wa seli mundu (siko seli).

Akizungumza na kituo hiki daktari wa magonjwa ya kibinaadamu kutoka Decca Pollyclinic Dkt Mettew Gaudance, amesema kuwa ugonjwa wa seli mundu umekuwa na dalili tofauti ambapo kwa watoto mara nyingi huwa na maumivu ya viungo na upungufu wa damu.

Ameongeza kuwa moja ya tiba nzuri kwa Wagonjwa wa selimundu ni kunywa maji kama sehemu ya tiba, ili kuruhusu mzunguko mzuri wa damu na kufika kituo cha afya kwa ajili ya tiba zaidi.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya Wakazi Jijini hapa kufahamu namna gani wanaelimu na muamko wao katika kupima ugonjwa huo, ambapo wamesema kuwa ni muhimu jamii ikaendelea kukumbushwa juu ya magonjwa hayo yasiyo ya kuambukizwa.

Ugonjwa wa seli mundu ambao kitaalamu hufahamika kama Sickle cell Ni ugonjwa wa kurithi ambao huonekana kwa wingi katika nchi za Afrika magharibi India na visiwa vya mediterania, Ugonjwa wa seli mundu husababisha ishara mbalimbali na madhara mwilini ikiwa pamoja na kuongezeka kwa hatari ya kupata maambukizi na kiharusi.