Dodoma FM

Wazazi watajwa kuwa chanzo cha watoto kuacha shule

7 March 2022, 1:28 pm

Na; Neema Shirima.

Imeelezwa kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa chanzo cha watoto wao kutokukwenda shule kutokana na kutowanunulia vifaa vya shule pamoja na sare za shule

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Hombolo bwawani bwn Andrew Mseya wakati akizungumza na taswira ya habari ambapo amesema wapo baadhi ya wazazi ambao wamekuwa wakisababisha utoro wa shule kwa watoto wao kwani wamekuwa wakishindwa kuwanunulia vifaa vya shule ikiwa ni pamoja na sare za shule

CLIP 1……………………DIWANI

Amesema katika kata yake amewaagiza viongozi wa mtaa wahakikishe wanafanya sensa ya nyumba kwa nyumba na kuhakikisha wanaorodhesha familia ambazo hazijawapeleka watoto wao shule ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kukiuka sheria ya kutokumtimizia mtoto haki yake ya kupata elimu

CLIP 2……………….DIWANI

Aidha kwa upande wa wazazi wamesema wakati mwingine watoto wanashindwa kuhudhuria shule kutokana na waalimu kuwa wakali ambapo pia wameahidi kushiriki kwa kiasi kikubwa katika kuwahimiza watoto wao kuhudhuria shuleni

CLIP 3…………….WAZAZI

Ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha mtoto anapata haki ya elimu kwa wakati anaostahili ili kumjengea mazingira mazuri kwa maisha yake ya baadae