Dodoma FM

Ubovu wa barabara wakwamisha baadhi ya shuguli za maendeleo

4 February 2022, 3:55 pm

Na; Victor Chigwada.

Kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha Jijini hapa maeneo mengi yenye barabara za kawaida hususani vijijini yamekuwa yakiathirika kwa kiasi kikubwa na hata kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeleo.

Wananchi wa Kata ya Loje ni miongoni mwa wahanga wa uchakavu wa miundombinu ya barabara na Dodoma Fm imefanya mazungumzo na baadhi yao na kuelezea hali halisi ya barabara yao

Mwenyekiti wa kijiji cha Loje Bw.Imanueli Idumo amekiri barabara yao kukosa marekebisho kwa muda mrefu na kuwaomba TARULA kuwasaidia  kufanya ukarabati

Naye Diwani wa Kata ya Loje Bw.John Njohoka amesema kuwa barabara imekuwa changamoto kubwa hali inayopelekea kukatika kwa  mawasiliano baina ya kijiji cha loje na vijiji jirani

Barabara nyingi za vijijini zimekuwa zikisahaulika katika kufanyiwa ukarabati na kusababisha adha hususani ifakapo msimu wa masika