Dodoma FM

Ugumu wa maisha unachangia tatizo la msongo wa mawazo kuongezeka

25 October 2021, 11:02 am

Na; Benard Filbert.

Kutokana na vijana wengi kujikita Zaidi katika shughuli za utafutaji wa Maisha pindi mipango hiyo inaposhindwa kukamilika imeelezwa kuwa husababisha tatizo la msongo wa mawazo.

Hayo yameelezwa na Nuru Julius ambaye ni mtaalamu wa saikolijia kutoka Chuo kikuu cha Dodoma wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu sababu za msongo wa mawazo hasa kwa vijana.

Nuru amesema zipo sababu nyingi ambazo zinasababisha msongo wa mawazo kwa vijana ikiwa pamoja na kujikita katika utafutaji wa Maisha na baadhi yao wanaposhindwa kutimiza mipango ndipo msongo wa mawazo huanza.

Bi Nuru amesema kutokana na vijana kuwa na vitu vingi vyakufanya katika umri huo wamekuwa wakipata msongo wamawazo pasipo wao kujua hivyo muda mwingine kukosa ufanisi wa fikra.

Mmoja wa kijana akizungumza na taswira ya habari amesema ni vema kipindi cha ujana kila mmoja akapangilia mambo yake vizuri ili kuepuka msongo wa mawazo ambao muda mwingine unaotokana na kuwa na vitu vingi kwa wakati mmoja.

Vijana wanashauriwa kuepuka vitu vinavyopelekea msongo wa mawazo ili kuepuka kupata magonjwa ambayo yatapunguza utendaji kazi hapo baadaye.