Dodoma FM

Asilimia 78 hadi 80 ya wakazi wa Dodoma wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya macho

20 October 2021, 11:28 am

Na; Yussuph Hans.

Imeelezwa kuwa kati ya Asilimia 78 hadi 80 ya wakazi wa Dodoma wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ya macho ikiwemo uoni hafifu.

Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka Hospitali ya Rufaa Dodoma, Dk. Msigaro Leah Erasto wakati akielezea hali ya magonjwa mbalimbali ya macho katika maadhimisho ya wiki ya afya ya macho Duniani.

Dk. Msigaro amesema  kuwa changamoto zipo nyingi katika Jamii na kwamba wengi bado hawana uelewa kuhusu afya ya macho pamoja na jinsi ya kuyalinda.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wananchi kufanya uchunguzi wa macho Bila kujali kuwa wana matatizo au la,ameongeza kuwa wanatakiwa kufanya uchunguzi kuanzia miezi sita hadi Mwaka.

Kwa upande  wao baadhi ya wafanyabiashara wa Stendi ya nanenane iliyopo jijini hapa wamewashukuru wataalam wa Afya ya macho kwa kuwatembelea na kuwapa huduma hiyo.

Haya yanajiri ikiwa ni Madhimisho ya siku ya afya ya macho duniani ambayo hufanyika kila alhamisi ya pili ya mwezi wa kumi ambapo lengo lake ni kuhakikisha uwepo wa huduma za macho zinazofikika kwa kila mwenye tatizo ,na kwa mwaka huu imebeba kauli mbiu isemayo “PENDA MACHO YAKO KILA MMOJA ANAHUSIKA NENDA KAPIME SASA”