Dodoma FM

Mwititikio wa chanjo katika kata ya zuzu walalamikiwa kuwa hafifu

19 October 2021, 11:10 am

Na; Shani Nicolaus.

Imeelezwa kuwa Pamoja na elimu inayoendelea kutolewa kwa baadhi ya maeneo nchini juu ya chanjo ya uviko 19 lakini mwitikio wa kuchanja katika kata ya Zuzu umekuwa mdogo.

Akizungungumza na Dodoma fm Diwana wa kata hiyo Mh. Awadhi Abdalah amesema kuwa upotoshaji umekuwa mwingi hali inayosababisha wananchi hao kuwa na hofu katika uchanjaji.

Amesema kuwa serikali ya kata imejitahidi kutafuta njia mbalimbali za kutoa elimu juu ya chanjo kwa kuweka mikutano ya hadhara , makanisani na kwenye shughuli mbalimbali lakini bado wanaona kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza elimu hiyo.

Ameongeza kuwa wananchi waache kusikiliza maneno ya watu badala yake wachukue hatua ya kuchanja kwani viongozi wengi wa kata hiyo wamechanja na hakuna madhara yoyote waliyoyapata.

Mara kadhaa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuchanja na jana katika hotuba yake akiwa Wilayani Longido aliwasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kupata chanjo.

Hata hivyo Jamii imeendelea kuhamasisha kuchukua tahadhari ya Uviko-19 huku wakitakiwa kujitokeza kwenda kupata chanjo ya ugonjwa huo.