Dodoma FM

Nzinje waipongeza serikali kwa kutatua changamoto za maji

28 September 2021, 1:18 pm

Na; Shani Nicolous.

Mwenyekiti wa mtaa wa Nzinje Bw .Godfrey Daud Samweli amepongeza juhudi mbalimbali za serikai zinazofanyika kutatua changamoto za mtaa huo.

Akizungumza na Taswira ya habari mwenyekiti huyo amesema kuwa kuna shughuli zinaendelea katika mtaa huo kama kusafisha kisima, kupima maeneo mbalimbali kwaajili ya nguzo za umeme na tayari bajeti imewekwa kwaajili ya kutengeneza kivuko mtaani hapo.

Amesema kuwa wananchi wanahitajika kuthamini na kujali jitihada zinazoonyeshwa na serikali kwa kutoa ushirikiano wa kutoksha ili kumaliza changamoto zinazo ukabili mtaa huo.

Taswira ya habari imemtafuta mkuu wa kitengo cha mawasiliano kutoka DUWASA Sebastiani Warioba ambaye amesema kuwa tayari kuna juhudi zimefanyika za kusafisha kisima kilichobaki ni umeme kwaajili ya usambazaji wa maji hayo.

Serikali kupitia Mh. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutatua baadhi ya changamoto nchini ikiwemo tataizo la maji ni jukiumu la kila Mtanzania kushiriki kwa kutunza na kulinda miundominu itakayo kuwepo katika maeneo husika.