Dodoma FM

Ripoti za matukio ya ukatili dhidi ya wanaume jijini Dodoma zaongezeka

27 September 2021, 12:08 pm

Na; Shani Nicolaus.

Imeelewza kuwa muitikio wa kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanaume jijini Dodoma umeongezeka.

Akizungumza na Taswira ya habari Afisa wa jinsia na watoto kutoka Kituo kikuu polisi Dodoma Maicko Nkinda Sabuni amesema kuwa kumekuwa na mwitikio mkubwa wa kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wananume kuliko zamani.

Amesema kuwa hali hiyo inaonyesha jinsi gani jamii imeanza kupata uelewa vizuri hivyo jitihada za elimu zinaonyesha kutoa matokeo chanya juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanaume.

Amesema kuwa pamoja na elimu hiyo Dawati la jinsia wameweka mazingira rafiki na wezeshi yatakayosaidia mlengwa kuwa huru kuzungumza kwa kutunziwa siri zake pamoja na chumba maalumu cha mhusika kuelezea ukatili anaofanyiwa bila wasiwasi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema kuwa mwanaume kutokuripoti ukatili sio jambo jema lakini sababu kubwa ni kukosa elimu juu ya dawati la jinsia kwani mpaka sasa watu wanafikiria dawati la jinsia ni kwaajili ya akina mama na watoto pekee.

Mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia katika jamii si suala la dawati la jinsia pekee bali ni jukumu la kila Mtanzania kupambania haki zake za msingi na kuripoti ukatili wowote anaofanyiwa mtu husika .