Dodoma FM

Zaidi ya asilimia 42 ya watoto Nchini wenye miaka 0 hadi 5 wamedumaa kutokana na lishe duni

27 August 2021, 1:24 pm

Na ;Fred Cheti .

Inaelezwa kuwa zaidi ya watoto 130 hupoteza maisha kila siku kutokana na lishe Duni hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2020 kutoka shirika la SEMA TANZANIA linalojihusisha na usimamizi wa haki za watoto
Pia inaeleza kuwa zaidi ya asilimia 42 ya watoto Nchini wenye umri wa chini ya miaka 0 hadi 5 wamedumaa kutokana na lishe duni kabla na baada ya kuzaliwa.

Taswira ya habari imezungumza na wakazi jijini hapa ili kufahamu ni kwa sababu gani wazazi au walezi wanashindwa kuwapatia watoto mlo ulio kamili ambapo wametaja sababu ya umasikini katika familia nyingi kuwa ni chanzo kikubwa.

Kwa upande wake Mtaalamu wa afya Kutoka kliniki ya Goldeni Gate Sanitarium Dkt. David Kavishe amesema jamii inahitaji kupatiwa elimu zaidi kuhusu kuwapatia watoto mlo kamili ili kuondokana na dhana ya kutowapatia watoto lishe bora kwa kisingizio cha umasikini kutokana na uwepo wa vyakula vingi vya asili ambavyo ni mlo kamili kwa mtoto.