Dodoma FM

TALGWU yatakiwa kusimamia maadili ya watumishi wake

24 August 2021, 1:41 pm

Na;Mindi Joseph .

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka amekitaka chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania TALGWU Kusimamia maadili ya watumishi wao ili kuondoa ukiukwaji wa maadili kwa watumishi Nchini.

Akizungumza leo jijini Dodoma katika mkutano mkuu wa taifa 2021 wa chama hicho amesema watumishi wanatakiwa kuzingatia maadili pamoja na kuwatetea watumishi wengine pale changamoto zinapojitokeza.

Ameongeza kuwa utumishi mzuri wenye matokeo lazima uwe na ufuatiliaji kwa watumishi wa ngazi zote.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wa serikali za mitaa tanzania Mwenyekiti wa chama Hicho Mkoa wa Mara Dkt Magreth Shawi amesema wataendelea kuzingatia weledi katika na maandili mahala pakazi.

Kesho Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh kasimu Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi Katika Mkutano huo wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania ambao unafanyika jijini Dodoma.