Dodoma FM

Shule ya msingi sokoni wilayani Bahi yakabiliwa na upungufu wa matundu ya vyoo

4 August 2021, 9:51 am

Na; Mariam Matundu.

Kukosekana kwa vyoo bora na rafiki kwa Wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Sokoni wilayani Bahi umesababisha wanafunzi kushindwa kujisitiri pale wanapohitaji kutumia vyoo hivyo.

Wanafunzi hao Wamesema wamekuwa wakipata magonjwa ya kichocho hasa kwa wanafunzi weye ulemavu wa afya ya akili kutokana na kutokuwa na vyoo maalumu kwa ajiliyao na vilivyopo kuwa na mazingira machafu ambayo kulingana na hali zao hawawezi kuchukua tahadhali.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wengine Yohana Stephano mwanafunzi wa darasa la saba mwenye ulemavu wa viungo ameiomba serikali kuboresha mazingira ya ujifunzaji kwa wanafunzi wenye ulemavu.

John Josephat ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sokoni amesema shule yake ina wanafunzi 11 wenye ulemavu wa aina mbalimbali na kwamba wanapata changamoto kubwa kutokana na ubovu wa vyoo hivyo vinavyotumika kwa sasa.
Aidha amesema wamepata ufadhili wa kanisa la FPCT ambapo wanajenga matundu ya vyoo kumi na tano lakini bado hayawezi kutatua changamoto hiyo kutokana na shule hiyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi.

Nae Diwani wa kata ya Bahi Sokoni kwa kushirikiana na wananchi wamekuwa wakishiriki katika ujenzi huo ili kutatua changamoto hiyo na kwamba bado anaendelea kutafuta wadau wengine ili kuendelea kutatua changamoto hiyo .