Dodoma FM

Wanaume na wavulana wahitaji elimu zaidi ili kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia

2 August 2021, 1:34 pm

Na;Yussuph Hans.

Ukatili Dhidi ya Watoto Tanzania: Muhtasari

Imeelezwa kuwa bado kuna ukimya unaoendelezwa na baadhi ya Wanaume na Wavulana wanaofanyiwa vitendo vya ukatili wa katika jamii hali ambayo inawasababishia madhara makubwa mbeleni.

Wakizungumza na taswira ya habari wakazi jijini Dodoma wamesema kuwa ili kupiga hatua katika mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, elimu bado inahitajika kwa wanaume kuhakikisha wanatoa taarifa za vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mkaguzi Msaidizi kutoka Dawati la kijinsia dodoma Jelda Luyangi amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa ujumla vimekuwa na Madhara kwa pande zote mbili ijapokuwa mara nyingi wanaume wamekuwa na ugumu katika kutoa taarifa za vitendo hivyo.

Naye Mwasaikoloji kutoka kituo cha kulea Watoto wanaishi katika Mazingira Magumu KISDET Mtahu Mtahu, amesema kuwa kuna kundi la Wanaume walioathirika na ukatili wa kijinsia na baadhi yao hufanyiwa vitendo hivyo na watu wao wa karibu.

Ukatili wa kijinsia ni kitendo chochote ambacho kinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na kutishiwa maisha, kunyimwa uhuru, iwe hadharani au kwa kificho.